Mahujaji wanne (4) kutoka nchini Tanzania wamethibitishwa kufa katika tukio la kukanyagana lililotokea jana huko Mina karibu na mji Mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakar Zuberi iliyotolewa
akiwa Makka, watanzania watatu waliokwisha tambuliwa majina yao ni pamoja na Mkungwe Suleiman Hemedi, Sefu Saidi Kitimla na Bi. Mwanaisha Hassan Juma.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mtanzania mwingine aliyekufa ambaye ni mwanamke, jina lake bado halijajulikana na kuna raia mmoja wa Kenya aliyefariki Bi. Fatuma Mohammed Jama, ambaye alisafiri kwenda Makka kwa kutumia wakala wa Tanzania.
Watanzania hao ni miongoni mwa mahujaji 717 kutoka sehemu mbalimbali duniani, waliopoteza maisha na wengine zaidi ya 800 kujeruhiwa katika tukio la kukanyagana, wakati wa kutimiza kipengele muhimu cha ibada ya Hija cha kumtupia mawe shetani.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment