Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli ametoa mpya nyingine katika mkutano wa hadhara ambapo amesema kwamba ile Peoples Power ya Chadema apewe yeye ili aweze kuwatumikia wananchi nchini Tanzania.
Aidha, Magufuli ni mgombea ambaye haishiwi vituko ikiwa ni katika mkutano wa kampeni mwingine aliamua kupiga push-up takribani saba kuwaonesha wananchi kuwa
yuko fiti kiafya,licha ya kupiga maozezi katika mkutano mwingine wa Kampeni Magufuli aliwaambia wananchi kuwa ile slogani ya Chadema ya M4C maana ni Magufuli for Change.
Hata hivyo suala la kuibadilisha slogani hiyo limepokelewa tofauti na viongozi wa Chadema ambapo wakizungumza na waandishi wa Habadri Chadema walidai wamepanga kumfikisha mahakamani kwa kuiba slogani ya chama kingine.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment