‘SUPA AJENTI’ JORGE MENDES ADAIWA KUTIA MKONO KUHARIBU DILI DE GEA KWENDA REAL!


JORGEMENDES-RONALDOJorge Mendes ni Wakala wa Watu maarufu kwenye Soka wakiwemo Jose Mourinho, Cristiano Ronaldo, Angel di Maria, Pepe, Radamel Falcao na David de Gea lakini sasa umeibuka uvumi mzito kuwa alitia mkono kuisimamisha Dili ya De Gea kuhamia Real Madrid kutoka Manchester United.
Taarifa hizo zinadai Mendes, Raia wa Ureno, hakuridhishwa na mgao wake kwenye Uhamisho huo.
Kawaida Ajenti wa Mchezaji huzoa Asilimia 5 ya Dili yenyewe ikiwa pamoja na Aslimia hiyo hiyo kwenye Mshahara wa Mchezaji lakini wakati mwingine huzoa zaidi ikitegemea na makubaliano na Klabu inayonunua Mchezaji.

Kuelekea Msimu huu mpya wa Soka, Akaunti ya Mendes imezidi kufura baada ya kukamilisha Dili za kuuzwa kwa Angel di Maria kwenda kwa Paris Saint-Germain kwa Dau la Pauni Milioni 44 na pia ule Uhamisho wa Pauni Milioni 32 wa Nicolas Otamendi kwenda Manchester City kutoka Valencia. 
Hivi sasa Jorge Mendes ana Listi ya Wachezaji wanaokaribia 100 ambao yeye ndio Wakala wao kupitia Kampuni yake GestiFute na thamani ya Wachezaji hao Sokoni wakiuzwa ni karibu Pauni Bilioni 1.
MENDES-SUPA-AGENT
Hakuna anaejua Mendes, mwenye Miaka 49, alifanya nini Usiku wa Uhamisho wa De Gea uliokwama Sekunde za mwisho baada ya Real kuchelewa kumsajili kwenye Mtandao wa FIFA wa Uhamisho wa Kimataifa, TMS [Transfer Matching System] na pia kwenye LFP, La Liga.
Zipo nadharia nyingi zinasambazwa huko Ulaya kumnyooshea kidole Mendes baada ya kuharibika kwa Dili ya De Gea.

Hivi sasa duru za habari huko Ulaya zinadai Mendes ameshamshauri De Gea kusaini Mkataba mpya ulioboreshwa na Man United kitu ambacho inasemekana De Gea ameshakikubali.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: