BAADA
ya kuchapwa 3-0 huko Misri katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi G la
AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, Tanzania, maarufu kama Taifa
Stars, Leo wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Nigeria.
Nigeria,
chini ya Kocha Sunday Oliseh, Mchezaji wa zamani wa Nchi hiyo, wao
waliifunga Chad 2-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi G waliyocheza
kwao.
Ili
kujitayarisha kwa ajili ya Mechi hii, Taifa Stars walipiga Kambi ya
Mazoezi huko Ulaya Nchini Turkey na Jana Kocha wa Taifa Stars, Charles
Boniface Mkwasa, alisema wao wako tayari kwa mtanange huu.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
TIKETI:
-MAUZO:
-Vituo:
(i) Ofisi za TFF - Karume , (iii) Mbagala – Dar live, (iv) Ubungo –
Oilcom, (v) Makumbusho – Stendi, (vi) Uwanja wa Taifa, (vii) Mwenge –
Stendi, (viii) Kivukoni- Feri, (ix) Posta – Luther House, (x) Big Bon –
Msimbazi Kariakooo
-Viingilio:
VIP A Tsh 40,000, VIP B Tsh 30,000, VIP C Tsh15,000, Rangi ya Machungwa
(Orange) Tsh 10,000, Rangi ya Bluu na Kijani Tsh 7,000.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Akiongea
na Wanahabari Jana katika Ukumbi wa Mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa
Karume Jijini Dar es Salaam, Mkwasa amesema: “Tumefanya mazoezi kwa
takribani siku kumi, vijana wako katika hali nzuri ya mchezo, uwezo
waanaouonyesha mazoezini ni wa hali ya juu na unatupa matumaini ya
kufanya vizuri”
Pia
Mkwasa alisema katika mpira hakuna kinachoshindakana na anatambua
Nigeria ni Timu kubwa Afrika, waliotwaa Ubingwa wa Afrika mara tatu,
lakini mpira wa sasa lolote linaweza kutokea na wao wamejiandaa vilivyo
kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mkwasa pia aliwaomba Watanzania kuja kuwapa sapoti Wachezaji Uwanjani kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.
Mechi
hii itachezeshwa na Waamuzi kutoka Nchini Rwanda ambao ni Louis
Hakizimana (Mwamuzi wa Kati) Honore Simba (Mwamuzi Msaidizi), Jean Bosco
Niyitegeka (Mwamuzi Msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza (Mwamuzi wa
Akiba) na Kamisaaa wa Mchezo ni Charles Kasembe kutoka Nchini Uganda
ambao wote tayari waliwaili Dar es Salaam tangu Juzi Jioni.
Mechi hii itaanza Saa 10 na Nusu Jioni, Saa za Bongo.
TANZANIA:
-KOCHA: Charles Boniface Mkwasa
-WACHEZAJI:
lly Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji
Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka, Nadri Haroub
“Cannavaro”, Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum
Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva, Farid Musa, John Bocco, Rashid
Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa, Mbwana Samatta.
NIGERIA:
-KOCHA: Sunday Oliseh
-WACHEZAJI:
Ikeme Onoro, Ezenwa Ikechukwu, walinzi Thomas Olufemi, Balogun Aderemi,
kwambe Solomon, Omeruo Keneth, Ekong William, Oboroakpo Austin, Akasi
Chima, na Madu Kingsley.
Wengine
ni viungo Ibrahim Rabiu, Muhamed Usman, Uzochukwu Izunna, Haruna
Lukman, Nwankwo Obiora, Igboun Emeka, washambuliaji Simon Daddy, Ujah
Anthony, Emenike Chinenye, Musa Ahmed, Aggreh Obus na Eduok Samuel.
REFA: Louis Hakizimana (Rwanda)
0 comments:
Post a Comment