Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter anachunguzwa na viongozi wa mashtaka nchini Uswizi.
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imesema Blatter anachunguzwa kwa tuhuma za kuhusika na usimamizi mbaya pamoja tuhuma nyingine za kutumia vibaya pesa.
Blatter amehojiwa na pia Ofisi yake imepekuliwa , Uchunguzi huo unahusu mkataba wa haki za utangazaji wa runinga ambao Bw Blatter alitia saini pamoja na aliyekuwa mkuu wa soka wa eneo la Caribbea Jack Warner mwaka 2005.
Bw Blatter pia anatuhumiwa kufanya malipo yasiyo halali” mwaka 2011 kwa rais wa shirikisho la soka Ulaya Uefa Michel Platini.
Mwezi Mei, maafisa saba wakuu wa Fifa walikamatwa Zurich kwa tuhuma za ufisadi kutoka kwa maafisa wa mashtaka nchini Marekani.
Blatter alishinda uchaguzi wa urais wa Fifa mara ya tano mfululizo Mei 29 lakini, baada ya tuhuma za ufisadi kukumba shirikisho hilo, alitangaza Juni 2 kwamba angejiuzulu ,Blatter anatarajiwa kuondoka wadhifa wake wakati wa mkutano mkuu wa Fifa Februari 26.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment