Mtikisiko 2015 wazinduliwa rasmi mkoani Iringa

 _DSC0112

Na mwandishi wetu,

 Iringa. MSIMU waburudani wa ‘mtikisiko’ unaoratibiwa na kituo cha redio cha ebony kilichopo mjini Iringa, umezinduliwa rasmi tayari kwa kuanza kutoa burudani kwa wakazi wa mikoa minne ya kusini mwa Tanzania ambapo kwa mwaka huu inadhaminiwa na kampuni ya mtandao wa simu za mikononi wa Tigo Mtikisiko ambao umekuwa ukipata umaarufu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007
kwa kauli mbiu zake ikiwamo ya mwaka huu isemayo “mtikisiko 2015 tumefika na Tigo ,dhima kubwa ya msimu huo umekuwa ukitumika kurudisha shukrani kwa wasikilizaji, na wateja wa kituo hicho cha redio. Akizungumza katika uzinduzi wa msimu wa mtikisiko uliofanyika katika kituo hicho cha redio na kurushwa moja kwa moja hewani,mwenyekiti wa kamati ya maandalizi BonnieNyatogo maarufu kwa jina la Bonnie Sly alisema kwa mwaka huu wanatarajia kufanya mtikisiko wa burudani katika mikoa ya Ruvuma Mkoani Njombe katika halmashauri ya mji wa Makambako, Mkoani Mbeya katika wilaya ya Mbeya Mjini, na mtikisiko wa mwisho utafanyika mkoani Iringa. Bonnie sly alisema kwa mwaka huu wamedhamiria kutoa burudani iliyosheni ubunifu kutokana na maboresho makubwa waliyoyafanya kwenye vifaa, na ongezeko la mkoa wa Ruvuma. “maboresho tuliyoyafanya mwaka huu ni pamoja na vifaa vya sauti vya kisasa, jukwaa la kisasa, wasanii wachanga na wazoefu,na mambo mbalimbali yanayohusu jamii” alisema Bonnie Sly. Mratibu wa msimu huo waburudani Edwin Bashir maarufu kwa jina la “Eddo”aliwashukuru wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye viwanja vinavyotoa burudani pamoja na wafanyabiashara na makampuni ambayo yamekuwa yakitoa ushirikino kwa kituo hicho cha redio cha ebony. -



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment