Taarifa zilizotufikia muda huu kwenye chumba chetu cha habari ni kwamba Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu Taarifa hizo zimesema Waziri Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga Mashariki kupitia chama cha Mapinduzi, mwili wake utawasili nchini Jumamosi ya Septemba 26 mwaka huu Marehemu Kombani alikuwa akiugua maleria kali Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu uliowapata Taarifa zaidi za msiba huo zitakujia hapa hapa - See more at: http://edwinmoshi.blogspot.com/2015/09/breaking-news-waziri-celina-kombani.html#sthash.OS2xYjdQ.dpuf
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment