Mgombea wa CHADEMA atiwa mbaroni Dodoma
JESHI
la polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia Mgombea Ubunge kwa tiketi ya
Chadema, Benson Kigaila pamoja na wenzake kumi ambao ni wafuasi wa chama
hicho.
Kauli hiyo ya kukamatwa kwa wafuasi hao pamoja na mgombea ubunge huyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi, David Misime alipokuwa akizungumza waandishi wa habari.
Misime
amesema Kigaila na wenzake kumi wanadaiwa kukamatwa kutokana na kufanya
maandamano bila kibali na kuzuia watumiaji wengine wa barabara
kushindwa kuendelea na shughuli zao.
Mbali
na kufanya maandamano bila kibali jeshi la polisi linadai kuwa wafuasi
wa Chadema walimshambulia askali polisi kwa kutumia chupa ya soda
kumpiga nayo kichwani sambamba na kufanya fujo kituoni.
Misime
amesema matukio hayo yalitokea jana majira ya saa 12:45 kutokea
barabara ya Jamatini na kituo cha polisi baada ya mgombea ubunge wa
chadema kumaliza mkutano wake wa kampeni katika eneo la stendi kuu ya
Dodoma.
Misime
aliwataja waliokamatwa kuwa ni Benson Kigaila mgombea ubunge Chadema,
Khadija Maula, Godfrey Manyanya mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Dodoma.
Wengine
ni Stellah Masawe, Hashimu Kilaini, Alex Thomasi, Prisca Mgaza,
Luckyson kweka, Aisha Urio, Pompey Remijo na Lawi Tumuza.
Kamanda
amesema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi wanaandaliwa jarada
kwa ajili ya kuwapandisha kizimbani siku ya kesho.
Kutokana
na hali hiyo kamanda Misime amesema kuwa jeshi litaendelea kuwakamata
na kuwachukulia hatua wanasiasa ambao watafanya kampeni zao ambazo ni za
kuvunja amani.
Hata
hivyo Misime hakuweza kumtaja jina askari aliyedaiwa kujeruhiwa na
chupa kichwani na wala hakutaka waadishi wakutane na askari huyo.
pamoja na mgombea ubunge huyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi, David Misime alipokuwa akizungumza waandishi wa habari. Misime amesema Kigaila na wenzake kumi wanadaiwa kukamatwa kutokana na kufanya maandamano bila kibali na kuzuia watumiaji wengine wa barabara kushindwa kuendelea na shughuli zao. Mbali na kufanya maandamano bila kibali jeshi la polisi linadai kuwa wafuasi wa Chadema walimshambulia askali polisi kwa kutumia chupa ya soda kumpiga nayo kichwani sambamba na kufanya fujo kituoni. Misime amesema matukio hayo yalitokea jana majira ya saa 12:45 kutokea barabara ya Jamatini na kituo cha polisi baada ya mgombea ubunge wa chadema kumaliza mkutano wake wa kampeni katika eneo la stendi kuu ya Dodoma. Misime aliwataja waliokamatwa kuwa ni Benson Kigaila mgombea ubunge Chadema, Khadija Maula, Godfrey Manyanya mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Dodoma. Wengine ni Stellah Masawe, Hashimu Kilaini, Alex Thomasi, Prisca Mgaza, Luckyson kweka, Aisha Urio, Pompey Remijo na Lawi Tumuza. Kamanda amesema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi wanaandaliwa jarada kwa ajili ya kuwapandisha kizimbani siku ya kesho. Kutokana na hali hiyo kamanda Misime amesema kuwa jeshi litaendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua wanasiasa ambao watafanya kampeni zao ambazo ni za kuvunja amani. Hata hivyo Misime hakuweza kumtaja jina askari aliyedaiwa kujeruhiwa na chupa kichwani na wala hakutaka waadishi wakutane na askari huyo
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko