Mazoezi Ya Kegel


kukojoa upesi

Katika ukurasa mwingine katika tovuti yetu tulijadili tatizo la kuwahi kufika kileleni au kumaliza tendo la ndoa upesi. Tuliona kuwa kuna dawa unazoweza kutumia kupunguza tatizo hili na tuliona kuwa kuna mazoezi ambayo unaweza kuyafanya yakakusidia kuongeza muda wako wa kufika kileleni. Leo tutazungumzia mazoezi ya  Kegel ambayo yana manufaa mengi kwa mwanamme (na mwanamke pia). Mazoezi haya yamepewa jina hilo baada ya mtu wa kwanza kuyaelezea, Arnold Kegel mwaka 1948
.

 Faida Za Kufanya Mazoezi Ya Kegel


Mazoezi ya Kegel yamethibitishwa kusaidia kuondoa matatizo ya kutokwa na mkojo bila kukusudia hali ambayo kwa wanawake hujidhihirisha zaidi baada ya uzazi. Kwa wanaume mazoezi haya husaidia taizo la kuwahi kufika kileleni au kwa maneno mengine kumaliza tendo la ndoa upesi. Yanawasaidia pia wanaume kuwa na uume unaosimama kwa nguvu zaidi (increased size and intensity of erections). Mazoezi haya huzisaidia jinsia zote mbili kupata raha zaidi wakati wa kufika kileleni (intensity of orgasms). Kwa wanawake, huwasaidia kukaza misuli inayozunguka uke, kitu ambacho ni muhimu sana hasa baada ya tendo la uzazi.

 Mazoezi Ya Kegel Ni Nini?


Ni mazoezi yanayofanywa kwa kurudiarudia kwa kukaza (kubana) na kuachia misuli inayopo kwenye uvungu wa pelvis. Misuli hii huitwa misuli ya pubbocoxygennus (PC) na ndiyo misuli inayofanya kazi ya kudhibiti ufanyanyaji kazi wa dhakari. Mazoezi haya pia huitwa Pelvic Floor Exercises au PC exercises. Eneo ilipo misuli hii ni  katikati ya kinena na mwisho wa uti wa mgongo.

misuli ya pubococcugeus

 Namna Ya Kufanya Mazoezi ya Kegel


Mazoezi haya hufanywa kwa namna nyingi na mara nyingine yakiambatana na vifaa maalumu. Hapa naelezea mazoezi rahisi yenye lengo kuu la kukusaidia kuimarisha misuli yako usitokwe na mkojo ovyo na uweze kuongeza muda wako wa kufika kileleni.
Ukiwa umesimama au umekaa, legeza viungo vyako vyote vya mwili, usikaze matako wala misuli yako ya miguu au ya tumbo. Kaza misuli yako ya uvungu wa sehemu nyeti kama vile unazuia mkojo usitoke. Ukiwa bado umeikaza misuli hiyo, hesabu sekunde 3 hadi tano kisha ilegeze (ukiweza kuhesabu sekunde zaidi ni vizuri zaidi). Fuata ratiba uliyopewa hapa chini kuendelea na mazoezi yako. Tazama video hapa chini kwa mfano wa kufanya mazoezi haya:

Wiki  1  mikazo 30 kwa siku
Wiki  2  mikazo 30 kwa siku – mara mbili kwa siku
Wiki  3  mikazo 45 kwa siku – mara mbili kwa siku
Wiki  4  mikazo 60 kwa siku – mara mbili kwa siku
Wiki  5  mikazo 75 kwa siku – mara mbili kwa siku
Wiki  6  mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku
Wiki  7  mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 30
Wiki  8  mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 45
Wiki 9 mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 60
Wiki 10 mikazo 90 kwa siku – mara mbili kwa siku ongeza mikazo 75
Wiki 10 mikazo 90 kwa siku – mara tatu kwa siku



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment