MTOTO ACHOMWA MOTO MBINGA


 


 Mtoto Mary Emmanuel mwenye umri miaka mitano mkazi wa mtaa wa Kipika wilayani Mbinga mkoani Ruvuma amekuwa akinyanyaswa kwa kunyimwa chakula na sasa amechomwa moto kiganja cha mkono wake wa kushoto  na shangazi yake aitwaye Anneth Nyoku kwa madai ya kuiba kipande  cha nyama.  Afisa  maendeleo ya jamii wa wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma Bi.Davina Maketa anazungumzia tukio hilo ambapo mtoto  huyo anadaiwa kunyanyaswa kwa kunyimwa
chakula na kupigwa na shangazi yake anayeishi naye aitwaye Aneth Nyoku anayedaiwa kumchoma moto mtoto huyo huku wananchi wakilaani ukatili huo.   Naye mtuhumiwa wa ukatili huo Bi.Anneth Nyoku amesema hakuwa na nia mbaya kumchoma moto mtoto huyo bali lengo ilikuwa ni kumuonya kuacha tabia ya wizi.  Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Revocatus Malimi amesema taarifa za tukio hilo bado halijafika mezani kwake na atalifuatilia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa huyo


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment