Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi ameingia katika headlines baada ya kushindwa kuendelea na mechi dhidi ya Las Palmas. Lionel Messi alilazimika kufanyiwa mabadiliko baada ya kuumia goti.
Lionel Messi alitoka nje kupatiwa huduma na kurudi uwanjani ila alishindwa kuendelea na mchezo, hivyo kocha wa FC Barcelona Luis Enrique alilazimika kufanya mabadiliko na kumuingiza Munir El Haddadi dakika ya 10 ya mchezo na Lionel Messi kwenda benchi. Lionel Messi alipata jeraha hilo baada ya kuchomekewa mguu na beki wa Las Palmas Pedro Bigas Rigo.
Mitandao mingi barani Ulaya imethibitisha Lionel Messi kuwa atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nane ambapo ni sawa na muda wa miezi miwili. Licha ya Lionel Messi kutolewa nje mapema, mechi hiyo ilimalizika kwa klabu ya FC Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 2-1 magoli ambayo yalifungwa na Luis Suarez, Jonathan Viera akiipatia Las Palmas goli la kufutia machozi dakika ya 88.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment