Lowassa alia na hujuma za Wapinzani


Mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa.
Mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa.
Mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa  ameonesha kusikitishwa  na kitendo cha alio waita  wapinzani kumuhujumu kwa  kuchana mabango na kuyatupa porini katika maeneo mbali mbali nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni za chama cha CUF Visiwani Zanzibar jana Lowassa aliyepewa dakika tatu kusema neno katika mkutano huo alisema  wamebaini kuwa wapinzani wao wanachana mabango na kuyatupa porini.
Kwa mujibu wa  Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia hivi karibuni   alisema maeneo ambayo mabango hayo yaliondolewa na kuharibiwa ni Jiji la Dar es Salaam, Zanzibar na Iringa.
Licha ya kutoa kilio hicho Lowassa alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hao, wawapigie kura yeye na Maalim Seif, huku akisisitiza `ushindi’ upo.
Katika kampeni hizo Dk. Maalim Seif  amewaahidi wananchi visiwani humo kuwa endapo atashinda ataurejesha mchakato wa rasimu ya Katiba ya wananchi yenye maoni ya wananchi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: