<a href='http://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a3aba3f4&cb=Math.random()' target='_blank'><img src='http://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=18&source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&cb=Math.random()&n=a3aba3f4' border='0' alt='' /></a> Hatimaye kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekemea kauli zenye kuwajengea hofu wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia wa uchaguzi mkuu ujao.
Hatua hiyo inafuatia Dk.John Pombe Magufuli kutoa mifano isiyoshabihiana na hali iliyopo nchini ikiwemo kufananisha Tanzania na nchi zenye machafuko.
Kwa mujibu wa taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari imemtaka mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mh. John Magufuli kufuta kauli zake ikiwemo ya kufananisha mchakato wa uchaguzi na vuguvugu la mabadiliko ya Libya pamoja na serikali yake kuwapiga risasi wahalifu wa kutumia silaha.
<a
href='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a09a5920&cb=Math.random()'
target='_blank'><img
src='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=19&source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&cb=Math.random()&n=a09a5920'
border='0' alt='' /></a>
Aidha kituo hicho kilichopo chini Mkurugenzi Mtendaji Dk.Helen
Kijo-Bisimba kimesema kauli hizo zinatoa vitisho kwa wapiga kura kinyume
na demokrasia kwa kuwa huwezi kufananisha mabadiliko ya kimapinduzi ya
Libya na umwagaji damu uliotokea huko na mabadiliko ya amani kwa kupitia
mchakato wa uchaguzi za kidemokrasia.Katika hatua nyingine taarifa hiyo imesema kuwa kauli hizo za mgombea huyo ni za kukemewa kwa kuzingatia nchi na chaguzi zinaongozwa kikatiba na Katiba inakinzana kabisa na kauli zilizotolewa na kiongozi huyo.
0 comments:
Post a Comment