BRENDAN RODGERS KUNG’OKA LIVERPOOL, ANCELOTTI KUTUA


BRENDAN-RODGERSUPO uvumi mzito kwamba Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers yupo hatarini kutimuliwa na Carlo Ancelotti kuchukua nafasi yake.
Lakini habari za ndani kutoka huko Anfield zimekanusha uvumi huu wa Meneja wa zamani wa AC Milan, Chelsea na Real Madrid, Carlo Ancelotti, kuchukua nafasi hiyo kama inavyonadiwa.
Ancelotti amekuwa hana kibarua tangu aondoke Real Madrid mwishoni mwa Msimu uliopita.
Liverpool wamekuwa na matokeo mabovu Msimu huu na wamekuwa hawajashinda katika Mechi zao 5 zilizopita na kuwaacha wakiwa na Pointi 8 tu kwa Mechi 6 za Ligi Kuu England
.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LIVERPOOL-Matokeo Mechi zao Msimu huuLigi Kuu England:
Agosti 2015
Ligi Kuu England:Liverpool 0-3 West Ham [Agosti 29]
Ligi Kuu England:Arsenal 0-0 Liverpool [Agosti 24]   
Ligi Kuu England:Liverpool 1-0 Bournemouth [Agosti 17]    
Ligi Kuu England:Stoke 0-1 Liverpool [Agosti 9]
Septemba 2015
Ligi Kuu England:Liverpool 1-1 Norwich [Septemba 20]  
Europa Ligi - Kundi B:Bordeaux 1-1 Liverpool [Septemba 17]   
Ligi Kuu England:Man United 3-1 Liverpool [Septemba 12]       
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Mechi inayofuata kwa Liverpool ya Ligi ni hapo hapo kwao Anfield hapo Jumamosi dhidi ya Aston Villa lakini Jumatano wapo pia Anfield kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup dhidi ya Timu ya Daraja la chini Carlisle.

@SOKA IN TANZANIA



Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment