WATANO WAFA KWA KUTUMBUKIA KWENYE MTO LUGARAWA LUDEWA MKOANI NJOMBE


Na Barnabas Njenjema LUDEWA

Watu watano Wanasadikika Kufariki  huku wengine wawili wakijeruhiwa kufuatia ajali ya gari iliyotokea Jana asubuhi katika wilaya ya ludewa mkoani Njombe Baada ya Kutumbukia Katika Mto Lugarawa.

Taarifa Toka Wilayani Ludewa Zinasema Kuwa  Ajali hiyo iliyo husisha gari aina ya TOYOTA Crasta Lenye namba za usajili T.613 AKA iliyokuwa ikitokea Lugarawa kwenda kijiji cha shaurimoyo wilayani ludewa imesababisha vifo vya watu Hao Ambao wamefahamika kwa majina ya ALONI HAULE (40) , PENDO MBAWALA (29) , WESLAUS MTWEVE (40) ,EDITHA HAULE (35) na PASCALIUS MLWILO (20) ambae ni mwanafunzi wa chuo cha Nursing Lugarawa.

Aidha taarifa kutoka eneo la tukio Zimesema kuwa katika ajali hiyo pia kuna watu wawili ambao  ni majeruhi wanaofahamika kwa

majina ya HURUMA MWINUKA na GERADO MWINUKA.

Hata Hivyo Chanzo Cha Tukio Hilo Bado Hakijafahamika Mara Moja na mtandao huu utaendelea Kufuatilia Zaidi Ili Kujua Chanzo Chake
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: