Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe Kelvin Ndimbo
Na Barnabas njenjema Ludewa
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limesema Limebaini Chanzo Cha Ajali ya Gari Iliyosababisha Vifo Vya Watu Watano Wilayani Ludewa Kuwa ni Mwendokasi Aliokuwa na Dereva wa Gari Hilo.
Akizungumza na Vyombo Vya Habari Ofisini Kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Amesema Kuwa Ajali Hiyo Iliyohusisha Gari Ndogo Yenye Namba za Usajiri T.613 AKA Aina ya Toyota Cresta Imeanguka Kwa Kutumbukia Katika Mto Baada ya Dereva Ambaye ni Alon Haule na Mmiliki wa Gari Hilo Kushindwa Kumudu Gari Kutokana na Mwendokasi Aliokuwa Nao na Kisha Kutumbukia Mtoni.
Kamanda Mutafungwa Amewataja Waliokufa Kuwa ni Pamoja na ALONI HAULE (40) , PENDO MBAWALA (29) , WESLAUS MTWEVE (40) ,EDITHA HAULE (35) na PASCALIUS MLWILO (20) ambae ni mwanafunzi wa chuo cha Nursing Lugarawa.
Katika Tukio la Pili Kamanda Mutafungwa Amesema Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limepokea Taarifa Toka Kwa
Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Malimbuli Kata ya Mang'oto Wilayani Makete Alex Ponela Baada ya Kugundua Kuwepo Kwa Mauaji ya Joshua Salum Sudy Maarufu Kwa Jina la Mwaka Ambaye Amekufa Baada ya Nyumba Yake Kuchomwa Moto Kwa Wizi wa Kimapenzi.
Hata Hivyo Wito Umetolewa Kwa Watu Kuacha tabia ya Kujichukulia Sheria Mkononi na Kusababisha Madhara Makubwa ya Vifo na Uhalibifu wa Mali Katika Maeneo Yao Jambo Ambalo ni Hatari Kwao
0 comments:
Post a Comment