Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewataka Walinzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo waliomlinda mgombea urais wa chama hicho Edward Lowassa alipowasili mkoani humo mnamo tarehe 14 agosti 2015 kujisalimisha Polisi kwa mahojiano.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani humo na kusainiwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Sacp Ahmed Msangi imebainisha kuwa katika msafara wa Lowassa kutoka uwanja wa ndege [songwe] kulionekana gari moja (pichani) aina ya Land Cruiser – Pick Up yenye rangi nyeusi na ndani yake lilikuwa limebeba vijana ambao walikuwa wamevaa mavazi meusi, Kofia – Bereti nyeusi na miwani nyeusi na mabuti.
Watu hao walikuwa na muonekano kama askari na shughuli waliyokuwa wakifanya ya kuongoza msafara, ulinzi na kazi nyingine zifanywazo na jeshi la Polisi
Kutokana na muonekano wao na shughuli walizokuwa wakizifanya ilikuwa ikitafsirika kuwa ni Jeshi lifanyazo kazi hizo ambalo halikuwa likifahamika.
Kutokana na sintofahamu hiyo wananchi wengi walikuwa wakihoji “hilo ni jeshi gani” sambamba na kutuma picha kwa njia ya mtandao wa kijamii [whatsapp] wakionyesha wasiwasi waliokuwa nao dhidi ya kikundi hicho.
Kufuatia hali hiyo, Ofisi Ya Mkuu Wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mbeya ilifungua jalada la uchunguzi ili kuwapata vijana wale kwa lengo la kuwahoji na kukamilisha upelelezi ili jalada lipelekwe kwa mwanasheria wa Serikali kwa ufafanuzi wa kisheria.
Jeshi hilo limedai kuwa hii ni kutokana na kuibuka kwa makundi ya aina hii hasa kwa vyama vikubwa vya siasa hapa nchini.
Katika kufanya ufuatiliaji huo, wapo watu wawili walikamatwa alfajiri ya tarehe 18.08.2015 Kwa mahojiano na baada ya maelezo yao kuchukuliwa walipewa dhamana.
Katika hatua nyingine taarifa hiyo imesema viongozi wao waliokuja Polisi wameelezwa kuhitajika kwa vijana wale waliokuwa katika gari lile ili wahojiwe na kukamilisha upelelezi wa jalada hilo Ili Mwanasheria wa Serikali alitolee mwongozo wa Kisheria
0 comments:
Post a Comment