Serikali yapiga marufuku Lowassa kutumia uwanja wa Taifa


Mgombew Urais Edward Lowassa.
Mgombea Urais Edward Lowassa.
Kufuatia UKAWA  kuomba kuzindua kampeni zake uwanja wa Taifa, Hatimaye Serikali  imetangaza
kupiga marufuku matumizi ya uwanja  huo kwa kile walichosema kuwa sio matumizi ya uwanja huo.
Akizungumza na wanahabari muda huu Jijini Mkurugenzi wa idara ya Habari maelezo Bwana Assa Mwambene  amesema kuwa ni kweli walipokea maombi kutoka CHADEMA tarehe 12 mwezi wa nane ya kuomba kutumia uwanja wa taifa mpya kwa ajili ya kuzindua kampeni na Tayari wameshawajibu kuwa hawawezi kuruhusu uwanja wa serikali kutumika kwa shughuli za kisiasa kwa chama chochote nchini.
Ameongeza  kuwa wameshangaa kuona taarifa mbalimbali kwenye magazeti leo zikisema kuwa kampeni ya CHADEMA itazinduliwa hapo wakati tayari serikali imeshapiga marufuku sehemu za serikali kutumika katika shughuli za kisiasa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: