Mchezaji wa klabu ya Yanga Malimi Busungu amesema kuwa siku zote alizokuwa kambini mkoani Mbeya amepata changamoto nyingi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu.
Amesema kuwa kambi hiyo iliweza kumfanya apate vitu ambavyo hajawahi kuvipata tangu alipoanza kucheza soka hapa nchini na kuahidi kuvitumia katika mchezo wao wa ngao ya jamii dhidi ya Azam na msimu huo.
“Kambi ya mbeya sio siri nimejifunza mambo mengi ambayo yatanisaidia kwenye mchezo wetu wa ngao ya hisani pamoja na mashindano ya ligi kuu msimu ujao naahidi kuvifanya vyote,”Amesema Busungu.
Ameongeza kuwa Kocha wao mkuu Han Van Pluijm anatumia mfumo mzuri ambao unamfanya aelewe haraka na kuweza kushirkiana kwa haraka na wachezaji wenzake kwa lugha za kimpira wanapokuwa uwanjani.
“Mfumo wa kocha nina uelewa wala haunisumbui kwa sababu naweza kuwasiliana vizuri na wachezaji wenzangu uwanjani na nje ya uwanja cha msingi mashabiki wetu wasichoke kutusapoti kwani wao ndio kila kitu,”alisema.
Aidha Amesema michezo ya kirafiki ambayo wameicheza imezidi kumjenga na kuyafanyia kazi makosa machache aliyoyabaini kwa upande wake kufuatia michezo hiyo mitatu.
0 comments:
Post a Comment