Urais 2015:UKAWA yatikiswa, Dr. Slaa abeba siri nzito

Dr.Wilbroad Slaa pamoja na Prof Ibrahim Lipumba.
Dr.Wilbroad Slaa pamoja na Prof Ibrahim Lipumba.
Umoja  wa katiba  ya wananchi UKAWA umetikiswa leo kufuatia Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba kutangaza kujizulu kwa madai ya kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo huku Naibu Katibu mkuu Chadema  Dr. Wilbroad  Slaa akiendelea  kuumiza  kichwa  umoja  huo.

Aidha, UKAWA iliyo onekana  kuimiza kichwa CCM usiku na mchana na sasa imeanza mpasuko mkubwa  baada ya Lipumba kuachia Ngazi huku Dr.Slaa akitangaza kuzungumzia hatma yake ukawa muda ukifika.
Uamuzi wa Prof. Lipumba kujiuzulu umepokelewa kwa masikitiko makubwa na wanachama wa CUF na Ukawa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Wakizungumza  haya ndio baadhi ya maoni ya wanachama hao;
Jumanne Jumanne dereva Daladala kutoka maeneo ya Posta amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za Prof. Lipumba kujiuzulu kwani alikuwa na matumaini makubwa na umoja huo lakini hivisasa ana baki kutazama tu mambo yanavyokwenda.
Anna Mwakibinga Mkazi wa Mnazi Mmoja amesema yeye kwa upande wake ni mwana chama wa CCM hivyo uamuzi huo Prof. Lipumba kung’atuka  anaona kama ni ukomavu wa demokrasia.
Jerome Haule mkazi wa Kariakoo  amesema kwamba hivisasa imani yake kwa vyama vya siasa imetoweka kwa kuwa  wanasiasa wa Tanzania hawaeleweki.
Mwajuma  Shabani  amesema kwamba ana tumaini vyama hivyo vitajipanga vizuri ili kuhakikisha kuwa  vina ondoa tofauti zao.
Katika hatua nyingine Maalim Seif ambaye ni Katibu mkuu wakati wa kutambaulishwa Edward Lowassa kama  Mgombea Urais alisema kwamba hajapata taarifa zozote za mwenyekiti huyo kujiuzulu lakini hata hivyo jana zilienea taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Prof.Lipumba ana mpango wa Kujiuzulu.
Kufuatia kukwama kwa mkutano wake  Prof. Lipumba na Waandishi wa Habari makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam mchana, ilipofika jioni Prof. Lipumba alijitokeza na kuzungumzia madai ya kuwa anataka kujiuzulu  kutokana na mamia ya wananchi kuzingira ofisi za CUF wakitaka kufahamau hatma ya kiongozi wao.
Licha Prof. Lipumba kukana madai lakini leo ametangaza rasmi kujiuzulu uenyekiti CUF  na kutangaza kuwa atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.
Kwa upande wa Dr Slaa, alipoulizwa kuhusu taarifa zilizozagaa kuwa maisha yake yapo hatarini kwa kuwa anatishwa, Dk Slaa alisema atalizungumzia muda ukifika.
Dk. Slaa aligombea urais mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili baada ya Rais Jakaya Kikwete na ndiye aliyekuwa akitajwa kuwania tena nafasi hiyo kupitia Chadema na Ukawa kabla ya  kumteua Lowassa.
Kwa mujibu wa Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Bw.Tulizo Hendrick amesema kwamba migogoro inayoikumba UKAWA  ni dhahiri kuwa  ni neema kwa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa wananchi wanapoteza imani na umoja huo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: