Profesa Lipumba amesema uamuzi wake unafuatia kushindwa kuafikiana na makubaliano yaliyofikiwa na vyama vinne shirikishi vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Amesema hafurahishwi na kufanya kile wanachokifanya wenzake kwa kuwa atakuwa anakwenda kinyume na makubaliano ya uongozi bora.
Vyama vinne vinavyounda umoja huo ni CUF, Chadema, NCCR Mageuzi na National League for Democracy (NLD).
Profesa Lipumba 63, amekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF kwa miongo miwili (1995 – 2015) na amegombea nafasi ya urais katika miaka ya 2000, 2005 na 2010
0 comments:
Post a Comment