Simba SC ilimalizana na mshambuliaji huyo wa zamani wa Coastal Union ya Tanga juzi.
Lyanga amesaini mkataba wa miaka miwili na leo anatarajiwa kuelekea Zanzibar kuungana na wachezaji wengine walioko huko wakijinoa chini ya Kocha Mkuu Muingereza, Dylan Kerr.
Kusajiliwa kwa Lyanga na kutapoza machungu ya Simba SC kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo, ambaye licha ya kumalizana na Wana Msimbazi, lakini klabu yake ikataka 'dau la rekodi' kumuachia.
Ndani ya siku tatu Simba SC inakuwa sasa imesajili wachezaji wapya watatu, wengine wakiwa ni kiungo Mzimbabwe, Justice Majabvi na beki Mrundi, Emery Nimubona.
0 comments:
Post a Comment