Kufuatia kutokea sintofahamu iliyopelekea mkutano wa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Waandishi wa Habari kuahirishwa hatimaye Prof. Lipumba amejitokeza na kukana kujiulu.
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuanzia jana zimeenea taarifa kuwa Prof. Lipumba amejiuzulu suala lililopeleka leo kuitishwa mkutano na Waandishi wa Habari katika ofisi zao zilizopo Buguruni jijini Dar es salaam lakini ghafla mkutano huo uliahirishwa.
Sababu ya kuahirishwa mkutano huo inadaiwa kuwa ni wazee kumtaka Prof. Lipumba kuwaeleza kile alichopanga kuzungumza na waandishi wa habari huku wakiamua kuitishwa kikao kati ya Prof. Lipumba na wazee wa chama hicho.
Akizungumza mara baada ya kufanya kikao na wazee hao Prof. Lipumba amesema kuwa hajajiuzulu na kuwataka wanachama kuhakikisha kuwa wanakijenga chama cha CUF.
Katika hatua nyingine wananchama mbalimbali wa CUF wali izingira ofisi hiyo wakitaka kufahamu hatma ya kiongozi wao kutokana na kuwepo taarifa za kujiuzulu katika mitandao ya kijamii hivyo baada ya Prof. Lipumba kuzungumza nao wali ridhia na kuondoka katika eneo hilo la ofisi za CUF.
0 comments:
Post a Comment