Manchester United na Barcelona zimefikia makubaliano ya Uhamisho wa Pedro lakini Barca wanataka Fowadi huyo abakie kwao hadi wamalize UEFA SUPER CUP Jumanne ijayo.
Klabu hizo mbili zimekubaliana Ada ya Uhamisho ya Pauni Milioni 18.1 ambayo itapanda kwa Pauni Milioni 4.2 kutokana na Bonasi mbalimbali za mafanikio ya Fowadi huyo.
Jumanne ijayo huko Tbilisi, Georgia, Barcelona, wakiwa Mabingwa wa Ulaya, wanapambana na Sevilla, Mabingwa wa EUROPA LIGI, kugombea UEFA SUPER CUP, ambalo ndio Kombe huanua Msimu mpya wa Mashindano ya UEFA kwa Klabu Barani Ulaya.
Wakiwa na pengo la kutoweza kuwachezesha Mastaa wao, Lionel Messi na Neymar, ambao walipewa Likizo ndefu Zaidi kwa vile waliziwakilisha Nchi zao kwenye Copa America huko Chile na ndio kwanza wamejiunga na Timu, Barca wanataka Pedro abaki hadi Wiki ijayo kuziba nafasi hizo.
Pedro, mwenye Miaka 28 ambae ameifungia Barca Bao 98 katika Mechi 318, binafsi ameafika kuhamia Man United na anatarajiwa kuziba pengo la Angel Di Maria ambae yuko njiani kuhamia PSG.
Ikiwa Pedro atatua Man United basi atakuwa Mchezaji wa 6 kutua huko katika kipindi hiki kuelekea Msimu mpya kufuatia wapya Memphis Depay, Matteo Darmian, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger na Sergio Romero.
0 comments:
Post a Comment