WAKATI Manchester United ikithibitisha kuuzwa kwa Fowadi wao Angel Di Maria kwa Paris Saint-Germain, Mpinzani wa Klabu hiyo kwenye Raundi ya Mwisho ya Mchujo kuingia Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI atatoka kwenye Timu 5 ambazo zishabainika.
Manchester United yathibitisha kumuuza Angel Di Maria
Manchester United imethibitisha kuuzwa kwa Fowadi wao Angel Di Maria kwa Paris Saint-Germain ya France.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Argentina alisainiwa na Man United Mwaka Jana kutoka Real Madrid kwa Dau la Rekodi ya Uingereza na aliichezea Mechi 24 huku 8 akitokea Benchi.
Akiwa na Man United, Di Maria alifunga Bao 4.
Man United kucheza na moja kati ya 5 UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mpinzani wa Manchester United atakuwa ni mmoja kati ya Club Brugge, CSKA Moscow, Lazio, Monaco au Rapid Vienna kwenye Raundi ya Mwisho ya Mchujo kuingia Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Droo ya Raundi hii ambayo itachezwa Agosti 18 na 19 na Marudiano ni Agosti 25 na 26 itafanyika Kesho Ijumaa kwenye Makao Makuu ya UEFA huko Nyon, Uswisi kuanzia Saa 7 Mchana, Saa za Bongo.
Kwenye Droo hiyo, Man United, ambao wanaanzia hatua hii, wapo Chungu Namba 1 na watapambanishwa na Timu 1 kutoka Chungu Namba 2.
Droo kamili ya kuweka Mechi za Raundi ya Mwisho ya Mchujo inahusisha jumla ya Timu 20 ambazo zimewekwa Mafungu Mawili.
FUNGU LA MAN UNITED [Njia ya Ligi]
CHUNGU NA 1: Bayer Leverkusen, Manchester United, Shakhtar Donetsk, Sporting Lisbon, Valencia.
CHUNGU NA 2: Club Brugge, CSKA Moscow, Lazio, Monaco, Rapid Vienna.
FUNGU LA PILI [Njia ya Mabingwa wa Ligi zao]
CHUNGU NA 1: FC Basel 1893, Celtic FC (SCO), APOEL FC (CYP), FC BATE Borisov (BLR), GNK Dinamo Zagreb (CRO)
CHUNGU NA 2: Maccabi Tel-Aviv FC (ISR), FK Partizan (SRB), Malmö FF (SWE), KF Skënderbeu (ALB), FC Astana (KAZ
0 comments:
Post a Comment