MGOMBEA UDIWANI KATA YA MNDINDI KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA AMPA GWALA FILIKINJOMBE

mgombea udiwani kata ya mundindi vitalino mlelwa
Mgombea udiwani Kata ya mndindi wilayani Ludewa mkoa wa njombe  kupitia Chama cha Chadema democrasia na maendeleo Chadema ndugu  Vitalino Mlelwa amesema ili maendeleo ya Kata ya mndindi yapatikane kwa haraka Kuna umuhimu wa kushikiana baina ya wananchi, viongoz wa Kata husika , pamoja na mbunge ambaye ni mchapa Kaz.


  Hayo aliyasema mapema wakati akichukua Fomu ya kuwania nafasi ya udiwani katika kata ya mndindi wilayani Ludewa mkoa wa njombe katika ofisi ya Kata ya mndindi.

Pia aliongeza kuwa nafasi ya udiwani ni fursa ya kuwakilisha wananchi katika ngazi mbali mbali ikiwepo katika baraza Kuu LA madiwani ngazi ya wilaya. 

"Fursa hiyo pia ya kuwakilisha Kata kwa upande wa Kata ya mndindi imeshindika kutokana na madiwan wote wanaoshika Kata hiyo sio wazawa wa mndindi hivyo kuto watendea haki wananchi wa mndindi  kwa kipind kirefu hivyo mnipe mimi vitalino mlelwa mzawa wa mndindi ili kuleta maendeleo ya kwel "" alisema vitalino mlelwa mgombea udiwani Kata ya mndindi. 

Akimwelezea mbunge WA jimbo LA ludewa Mh. Deo filikunjombe ndugu Vitalino Mlelwa alisema kwa upande wake Hana shidah na mbunge kwa kuwa ni mchapa Kaz ndani na nje ya wilaya ya ludewa hivyo atapenda kufanya Kaz na mbunge mchapa kazi.. 

Kwa upande wa WANANCHI wa Kata ya mndindi wamempokea kijana wao na kusema kuwa ni mfano mzur Wal kuigwa kwa vijana wengine wote wa wilaya ya ludewa wanao kaa Mjini kurudi nyumbani kwa ajir ya kuleta maendeleo ya Kata husika.... 

"vijana wetu tumewasomesha ni vyema mkaja kututumikia wazaz wenu na jamii ya wana ludewa kijana nakuomba kuwa mzalendo usikubali kununuliwa "alisema mkazi wa Kijiji cha Aman Kata ya mndindi. 

Nao baadhi ya wakazi wa mndindi wakieleza hatua iyo wamesema kuwa wamefurahishwa na ujio wa kijana vitalino mlelwa ili kuongezaa chachu ya ushindani wa kweli katika uchaguz mguu  ujao.
ndugu mlelwa alisikitika kuwa Kata ya mndindi ndio Kata pekee yenye utajiri mkubwa wa madini ya Aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Chuma kwa kijiji cha mndindi na dhahabu kwa kijiji Aman wilaya ya ludewa. 

Lakin had hivi Sasa Kata hiyo haina kituo cha Afya cha uhakika pamoja na Elimu duni ya shule ya Kata hiyo ambayo haiendan kabisa na utajiri wa Kata hiyo... 

"wana mndindi tunashangaa madini yanafanyiwa uchaguzi miaka yote had hii Leo mwaka WA kumi ila hakuna tunachofaid had hiv Sasa "
Aliongeza mgombea huyo...
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: