Ikiwa saa kadhaa zimebaki kufanyika kwa mkutano wa mgombea Urais wa Ukawa Edward Lowassa kuomba wadhamini jijini Mbeya, Jeshi la Polisi limetangaza kupiga marufuku maanadamano hayo.
Kwa mujibu wa barua ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Z.Msangi imepiga marufuku kufanyika maandamano na kuutaka UKAWA kufanya mkutano tu.
Katika barua hiyo imewataka wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki. huku akisisitiza kuwa ieleweke si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Lowassa atawahutubia wananchi ikiwa ni katika mchakato wa kusaka wadhamini ikiwa ni moja ya sharti la Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa wagombea wa vyama vyote kutafuta wadhamini katika mikoa kumi ya Tanzania bara.
Sifa za wadhamini ni pamoja na kuwa wamejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura zoezi lililomalizika nchini kote siku kadhaa zilizopita
0 comments:
Post a Comment