MESSI, NEYMAR WAIPA BARCA GAMPER TROPHY!

BARCA-TRIO-MSNBao za Neymar na Lionel Messi za kipindi cha kwanza Jana ziliipa Barcelona Gamper Trophy walipoitwanga AS Roma ya Italy 3-0 huko Nou Camp Jijini Barcelona, Spain.
Mastaa hao wawili walijiunga na Barca Juzi tu kutoka Vakesheni hawakuonyesha kutu yeyote kwa kuchelewa kuanza mazoezi.
Bao la Neymar lilifungwa Dakika ya 25 baada krosi ndefu ya Messi kumkuta Jeremy Mathieu aliemshushia Neymar na kufunga.
Messi alifunga Dakika ya 40 alipolishwa vizuri na Neymar.

Bao la 3 la Barca lilifungwa Dakika ya 66 na Rakitic.
Huko nyuma Barca walikuwa wakitumia Mechibya Kombe lao Gamper Trophy mahsusi kutambulisha Wachezaji wao wapya kwa ajili ya Msimu mpya kwenye Mechi hii inayochezwa kwao Nou Camp lakini Jana wapya wao, Arda Turan na Aleix Vidal, walilazimika kubaki tu Jukwaani kama Watazamaji kutokana na Barca kuwa kwenye Kifungo cha FIFA cha kutosajilu Wachezaji wapya hadi Januari Mwakani.
Mechi zijazo kwa Barca ni Jumanne ijayo huko Tbilisi, Geargia ambayo wao kama Mabingwa wa Ulaya watawavaa Mabingwa wa Europa Ligi Sevilla, pia ya Spain, katika Mechi maalum kuashiria Msimu mpya wa UEFA ya kugombea UEFA SUPER CUP.
Kisha Barca watarudi kwao Spain kucheza Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya huko Spain ya kugombea Spanish Super Cup dhidi ya Athletic Bilbao anbayo huchezwa kwa mikondo miwili ya Nyumbani na Ugenini.
Barca watakutana tena na Bilbao kwenye Mechi yao ya kwanza kabisa ya utetezi wa Taji lao la La Liga hapo Agosti 23.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: