MABINGWA wa England, Chelsea, wakicheza kwao Stamford Bridge huko London Mechi yao ya mwisho ya Kirafiki ya michuano ya International Champions Cup kabla Wikiendi hii kuanza kutetea Taji lao la Ubingwa kwenye Ligi Kuu England, wamefungwa Bao 1-0 na Fiorentina ya Italy.
Fiorentina, ambayo Juzi iliwabwaga Mabingwa wa Ulaya Barcelona Bao 2-1 katika Mechi ya International Champions Cup, waliingia Stamford Bridge wakiwa na Kikosi kilichobadilishwa Wachezaji 7.
Bao la ushindi kwa Fiorentina lilifungwa na Gonzalo RodrÃguez katika Dakika ya 34 baada ya Kipa Begovic kulitema Shuti la Alonso na Rodriguez kumalizia.
Jumamosi, wakiwa hapo hapo kwao Stamford Bridge, Chelsea, ambao maandalizi yao hayakuleta matokeo ya kuridhisha baada kupokea vipigo kadhaa, wataanza utetezi wa Ubingwa wao kwa kucheza Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya wa 2015/16 na Swansea City.
VIKOSI:
Chelsea: Begovic, Cuadrado, Zouma, Terry, Aina, Mikel, Loftus-Cheek, Traore, Oscar, Moses, Falcao
Akiba: Courtois, Blackman, Ivanovic, Azpilicueta, Cahill, Matic, Fabregas, Ramires, Hazard, Willian, Remy
Fiorentina: Sepe, Rodriguez, Junior, Tomovic, Alonso, Vecino, Fernandez, Suarez, Roncaglia, Rebic, Babacar.
Akiba: Tatarusanu, Lezzerini, Hegazy, Bagadur, Badelj, Joaquin, Valero, Ilicic, Bernardeschi, Fazzi, Rossi
SORCE SOKA IN TANZANIA
0 comments:
Post a Comment