Mashabiki wa klabu ya simba wameonyesha kioja baada ya kumlilia aliyekuwa kipa wao Ivo Mapunda mara baada ya kusikia ameachana na klabu hiyo ya msimbazi yenye makao yake makuu Jijini Dar es Salaam.
Sakata hilo llizuka juzi jumatatu baada ya uongozi huo kukutana na ivo na kumueleza kuvunjwa kwa mkataba wake hali ambayo ilishtua wengi.
Wakizungumza na Hivisasa leo kwa nyakati tofauti na mwandishi wa gazeti la majira mashabiki hao walionekana kuumizwa na uamuzi uliochukuliwa na uongozi mpaka kumvunjia ivo ulaji wake.
Abdala Athumani ambaye alijitambulisha kama mwanachama wa timu hiyo alisema ivo msimu uliopita alijitahidi licha ya timu yao kushika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu.
Amesema uongozi huo utamkumbuka mchezaji huyo kutokana na umuhimu aliokuwa nao na kuwataka kufanya majadiliano na mashabiki kabla ya kuchukua uamuzi.
“Ivo ameniumiza kwa sababu msimu uliopita alitusaidia sana japokuwa timu yetu ilishika nafasi ya tatu kwa staili hii tutapoteza wachezaji wengi wazuri,”amesema Abdalla.
Kwa upande wake Mapunda aliipa baraka klabu hiyo kwa kusema imempa nafasi ya kutafuta maisha ya mbele kisoka tofauti na kuendelea kubaki sehemu moja.
“Naikshukuru na mungu azidi kuipa mafanikio simba naamini hii ni njia nzuri kwangu nitazidi kujitangaza zaidi nikiwa kama mchezaji bora ninayejiamini,”Amesema
0 comments:
Post a Comment