MAONI YA WANANCHI KURA ZA MAONI LUDEWA KUPITIA CCM


 


LUDEWA

Wananchi wialayani Ludewa katika mkoa wa njombe wamekuwa na maoni tofauti juu ya matokeo ya kura ya maoni ndani ya CCM yaliyotangazwa hivi karibuni na katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi ccm wilayani hapa bw,Enzi Elias.

Wakizungumza na redio best fm hivi karibuni wananchi hao wamesema kuwa wanakubaliana na matokeo ambayo chama cha mapinduzi ccm kimetangaza kwa kura tofauti kwa wagombea watatu akiwemo Deo filikunjombe,Injinia chaula na Capten Mpangala na kusema kuwa kila jambo ni lazima liwe na matokeo.

 
Aidha wananchi hao wamesema kuwa wagombea ambao wamemfuata filikunjombe kwa kupata kura ni muhimu kutambua kuwa hayo ni matokeo pamoja na kusema kwamba wao kama wagombea wachukue kama changamoto kutokana na matokeo hayo kwani kila mgombea alikuwa na wakala wa kusimamia zoezi hilo.

Hata hivyo wananchi wamesema kuwa filikunjombe amepata kura nyingi kutokana na shughuli ambazo alizifanya katika kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi wake huku wakiongeza kuwa wao kama wagombea ambao wamepata kura tofauti na filikunjombe ni vizuri wakawa washauri wa mgombea huyo.
via.best fm radio ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: