26MBARONI LUDEWA

Mahakama ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Hapo jana Agost 4 mwaka huu iliwahukumu watu 26 wakazi wa kata cha Mlangali kwenda jela miezi mitatu kila mmoja na kulipa faini kwa kosa la kufanya maandamano  katika Kituo cha Polisi Mlangali kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Ludewa mh Fredick Lukuna mbele ya mwendesha mashtaka ASP Mutairuka na kueleza kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 2 mwezi wa 7 mwaka 2014.

Aidha katika kosa la pili washtakiwa hao wametakiwa kulipa faini ya sh.laki 200,000 na atakayeshindwa anatakiwa kwenda jela miaka miwili kutokana na kuharibu vibaya mali za kituo cha polisi Mlangali na kuvunja vioo vya gari la RCO.

Hata hivyo hakimu amesema mara baada ya washtakiwa kumaliza kifungo hicho amewataka kulipa fidia ya sh.38,470 kama sehemu ya fidia ya vitu vilivyoharibika ambapo vitakabidhiwa katika idara ya ulinzi na usalama wilaya ya Ludewa.
VIA www.njenjenews.blogspot.com
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: