Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ni mgombea Urais kupitia UKAWA anatarajia kuwahutubia wananchi katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi (kesho tarehe 15).
Akizungumza na Vyombo vya Habari Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alisema kuwa mapokezi hayo yamekamilika kwa asilimia mia moja. Lengo la ujio huo ni kumtambulisha mgombea urais ambaye ataambatana na mgombea mwenza Juma Duni Hajji.
Licha ya kumtambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha pia kwa ajili ya kupata udhamini wa huku zoezi la udhamini likiwa limeshaanza mkoani humo.
Baada ya mkutano huo kuisha msafara huo utaelekea katika jimbo la Monduli ambapo pia Mh.Lowassa atapata wasaa wa kuhutubia wananchi katika jimbo hilo.
Viongozi watakaokuwepo katika msafara huo ni Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe, wenyeviti wenza wa ukawa kutoka NLD, NCCR pamoja na chama cha CUF, John Mnyika, Nibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na viongozi wengine.
Amesisitiza kuwa kwa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na vikosi vya usalama suala la Amani,Utulivu, Ulinzi na Usalama vitadumishwa katika msafara huo pamoja na mkutano huo.
Naye Naibu katibu mkuu wa Timu Lowassa for president Ndama Jeuri alisema wamejiandaa vizuri kumpokea na wataendelea kuhamasisha watu kumuunga mkono Lowassa
0 comments:
Post a Comment