LUDEWA
Barnabas Njenjema
Wanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)wilaya ya Ludewa katika mkoa wa njombe wameandamana hadi ofisi za chama hicho wilayani hapa kupinga uamuzi wa chama hicho kumpitisha Mgombea ambae wao kama wanachama hawamuungi mkono.
Uongozi wa chadema Umemteua ndugu. Bathromew Msambichaka mkinga kuwa mgombea ubunge wa chama hicho na kumuacha ndugu, Okol haule ambaeye ndiye alikuwa chaguo la wanachama wa chadema wilaya ya ludewa hapa mkoani Njombe.
mabadiliko hayo ya mgombea wa ubunge kwa chama cha chadema yamefuatia mara baada ya kubainika kuwa ndugu ocol haule alitumia njia zisizo rasmi kuweza kushinda katika uchaguzi huo.
Wakizungumza katika eneo la ofisi za chama hicho wanachama hao wamesema kuwa walikuwa na imani na chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kwa kile kilichoonekana kwa mgombea okol kushinda kwa kura nyingi dhidi ya msambichaka lakini kutokana na kukatwa kwa jina hilo wanachama hao wapo tayari kumfuata ndugu okol endapo atahamia chama cha Act-wazalendo.
Aidha mara baada ya wanachama hao kutoka katika ofisi za chama hicho walielekea katika eneo la soko na kufanya mkutano na mgombea ubunge huyo ambaye alikatwa jina hilo na ametangaza rasmi kuwa anahamia chama cha Act-wazalendo huku mgombea huyo akichoma kadi yake ya chadema pamoja nguo,kofia na vitmbaa na baadhi ya wanachama wa chadema kuchoma kadi hizo na kuhamia Act.
kamati kuu ya chadema mapema wiki hii ilitangaza majina ya wagombea wa ubunge katika nchi nzima huku kwa upande wa wilaya ya Ludewa aliteuliwa ni B ATHROMEO MKINGA huku kwa mkoa mzima wa Njombe wagombea wake ni kama ifuatavyo...
Njombe
Njombe Kusini EMMANUEL MASONGA
Lupembe (Njombe Kask) EDWIN E SWALE
Wanging’ombe DISMAS A LUHWAGO
Makete JACKSON T MOGELA
Ludewa ATHROMEO MKINGA
Makambako ORAPH MHEMA
barua ikionyeshwa kwa wanahabari na wanachadema