Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha vikali taarifa zilizo enea katika mitandao ya kijamii kwamba mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli atawagawia Laptop walimu wote nchini Tanzania endapo akichaguliwa kuwa Rais.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kwamba Mgombea urais wa chama hicho hajawahi kusema kuwa atawagawia walimu laptop sehemu yeyote ile.
Ameongeza kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji na zimetolewa na wananchi wenye malengo mabaya kwa kuwa muda wa kufanya kampeni bado haujatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yenye makao makuu jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment