Boda Boda zimeacha Kazi na Kumsindikiza Mwenzao
Msafara wa Boda Boda Kuelekea Makaburini
Gari hii ilitaka leta Mushike hapa baada ya kutaka kuchomekea
Gari lililobeba Mwili wa Marehemu likielekea Makaburini
Boda Boda zikiwa zimepaki Jirani na Makaburini
Makaburini
Jeneza la Marehemu Mahela
Msemaji kwa niaba ya Familia akitoa Mwongozo
Maandalizi ya Mazishi
Mazishi
Baadhi ya waombolezaji
Picha na Mbeya yetu
MAMIA ya wakazi wa Sae jijini
Mbeya wamejitokeza kwa wingi kumzika aliyekuwa mwendesha boda boda (pikipiki)
aliyefahamika kwa jina la Bahati Mahela (23).
Marehemu alipatwa na mauti wakati anapatiwa matibabu hospitali ya Rufaa
jijini Mbeya baada ya kuchomwa kisu shingoni na mtu ambaye hakuufahamika ambaye
alizikwa katika makaburi ya Halmashauri Mlima James Veta jijini Mbeya.
Kamanda
wa Polisi alithibitisha
kutokea kwa tokio hilo na kuongeza kuwa lilitokea tarehe 10.08.2015
majira ya saa mbili usiku huko eneo la Ituha baada ya marehemu
kukodishwa na abiria asiyemfahamu kutoka kijiwe cha Sae kwenda shule ya
Msingi
Ituha na ndipo wakiwa njiani alichomwa kisu shingoni na kisha kumpora
pikipiki
yake yenye namba za usajili MC 851 ABG aina ya Kinglion.
Alisema kufuatia tukio hilo
msako umefanyika na pikipiki imepatikana ikiwa imetelekezwa eneo la Uyole na
chanzo cha kifo chake ni kutokwa damu nyingi baada ya kuchomwa kisu shingoni na
kiini cha tukio hili ni kuwania mali.
Alisema upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na
kumtafuta aliyehusika katika tukio hilo.
Kwa upande wake baadhi ya
viongozi wa chama cha Bodaboda (UWABOM) walilaani vikali vitendo hivyo na
kuongeza kuwa Jeshi la Polisi linapaswa kusaidiana na madereva hao ili kumpata
mharifu.
0 comments:
Post a Comment