Sintofahamu imeendelea kugubika ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kuhusiana na Hatma ya Katibu mkuu wa Chadema Dr. Wilbroad Slaa aliyetofautiana na chama hicho kufuatia Mwanasiasa Edward Lowassa kupewa ridhaa ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe hivi karibuni aliwaambia wafuasi wa Chadema na Ukawa kwa ujumla kwamba kumekuwepo na kutokuelewana kati ya Katibu Mkuu ambaye ni Dr.Slaa pamoja na Wanchama wa Chama hicho kutokana na ujio wa Lowassa.
Mbowe alinukukiliwa akisema Chama cha Chadema hakiwezi kuwa chama cha kuhubiri mabaya ya jana na kuacha kujadili maendeleo ya kesho,hivyo kama kuna mtu hakubaliani na maamuzi ya chama hicho akae pembeni atafakari kwa kina kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla.
Licha ya Kauli hiyo Hivi karibuni Dr. Slaa alisema kwamba muda utakapofika atazungumza kila kitu hivyo kuwataka wananchi na wanachama kusubiri uamuzi huo.
Katika hatua nyingine Dr. Slaa ameweka kauli tata kupitia ukurasa wake wa Twita zinazozua minong’ono katika jamii huku baadhi ya wanachi wakisema kwamba huenda Dr.Slaa akabwaga manyanga kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba aliyetangaza kujiuzulu na kutimkia nchini Rwanda kufanya utafiti wa maendeleo.
Wakizungumza na mtandao wa Hivisasa baadhi ya wanachi na wanachama wa UKAWA wameonekana kutofurahishwa na maamuzi hayo ya Dr.Slaa kukaa pembeni huku wanachama wa CCM wakiwaombea njaa UKAWA kama ambavyo ule msemo wa “adui yako muombee njaa” unavyotanabaisha.
Hizi ni baadhi ya kauli za Dr.Slaa,…
Kutokana na kauli hizo nini hasa hatma ya Dr.Slaa Chadema pamoja na UKAWA kwa ujumla? Mimi na wewe hatujui hebu tusubiri kama alivyoa ahidi muda ukifika ataweka wazi msimamo wak
0 comments:
Post a Comment