Uteuzi huo unakuja siku chache baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kutoa ratiba ya mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018, Malawi ikipangwa kuanza na Tanzania, Taifa Stars katika mchujo wa awali.
Mtawali amepewa Mkataba wa mwaka mmoja akirithi mikoba ya mchezaji mwingine wa zamani wa kimataifa wa Malawi, Young Chimodzi aliyefukuzwa Juni mwaka huu baada ya The Flames kufungwa nyumbani 2-1 na Zimbabwe katika mechi ya Kundi L kufuzu Fainali za Mataiofa Afrika mwaka 2017.
Rais wa Chama cha Soka Malawi, Walter Nyamilandu amemtambulisha Mtawali sambamba na Msaidizi wake, Nsanzuwrimo Ramadhan katika Kituo cha Ufundi na Maendeleo cha Chiwembe mjini Blantyre leo asubuhi.
Nyamilandu amewaambia Waandishi wa Habari kwamba Mtawali amepewa jukumu la kuhakikisha The Flames inafanya vizuri katika mechi za kufuzu AFCON 2017 pamoja na Kombe la Dunia 2018 na Mtawali amefurahia changamoto hiyo mpya
0 comments:
Post a Comment