Wanaoshirikiana na majambazi wakamatwa jijini Dar Es Salaam

Watoto wawili wenye umri kati ya miaka kumi na kumi na moja na ambao hawajajulikana majina yao wamekamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Bunju nje kidogo ya jiji Dar-es-Salaam wakidaiwa kutumiwa na majambazi kuiba kwenye maduka ya huduma za simu na vipodozi huku watu wanaodaiwa kuwatuma kutoonekana hata baada ya kusakwa katika eneo hilo.

Wakizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio baadhi ya wamiliki wa maduka hayo wamesema tukio hilo la limewashangaza watu wengi kwakuwa majambazi hayo yametumia mbinu mpya ya kukata dari la majengo hayo kuingia katika dari wakisubiri wamiliki wa maduka waondoke jambo ambalo limezua hofu kwa wakazi hao.
 
Aidha wa wananchi hao wameliomba jeshi la polisi kufika haraka wanapoitwa katika matukio lakini pia kushirikiana na vikosi vya ulinzi shilikishi kufanya doria mara kwa mara katika mitaa yao na kuwaondoa vijana wanaoshinda vijiweni na kutumbukia katika uvutaji wa bangi na uporaji.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: