Shule yafungwa kwa zaidi ya miezi miwili kwa kukosa choo.

Katika hali isio ya kawaida shule ya msingi juhudi wilaya Morogoro imefungwa kwa  zaidi ya miezi miwili kutokana na kukosa choo ambapo  wazazi wamelazimika kuchangishana na kujenga matundu ya vyoo lakini hadi sasa serikali haijafungua shule hiyo huku wanafunzi wakizagaa mitaani kwa zaidi ya miezi miwili bila kusoma.

Wakizungumza kwa jaziba wazazi  wananchi  wa kijiji cha Mtego wa Simba ilipo shule hiyo  wamemlalamikia kuwa baada ya shule kufungwa wamelazimika kuchangishana fedha na kutengeneza matundu ya vyoo 13 lakini hadi sasa shule haijafunguliwa huku walimu wanaonekana wakizagaa mitaani na wakiendelea kupokea mishahara bila kufanya kazi ambapo wazazi hao wametishia kuhamisha watoto wao endapo serikali haitafungua shule hiyo.
 
Naye afisa elimu wa wilaya ya Morogoro Bw.Donald Pambe akijibu tuhuma za malalamiko ya wazazi amesema ni kwelishule zilifungwa kwa utaratibu kutokana  na kukosa matundu ya choo lakini ameahidi kutuma timu yake kufanya ufuatiliaji.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: