UKAWA yamsafisha Lowassa, maamuzi Magumu yanukia




Mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu  Edward Lowassa.
Mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.
Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Umemsafisha Mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu  Edward Lowassa aliyejiuzulu kutokana na  kashfa ya Richmond mwaka 2008.

Wakizungumza wakati wa kumkaribisha Edward Lowassa leo ndani ya  umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA katika ofisi za CUF zilizopo Buguruni jijini Dar es salaam viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wakiongozwa na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia wamesema  Lowassa  ni mtu makini, mfuatiliaji  wa karibu wa utendaji na pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuhamasisha umma kuikataa CCM na mifumo yake.
Naye Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumb amesema masuala ya ufisadi ni mfumo uliopo huku akihoji tangu lowassa jiuzulu je  ufisadi umepungua au umeongezeka, Hata hivyo amesema Lowassa mwenyewe alizungumza kwamba kama kuna mtu ana ushahidi yeye ni fisadi autoe ushahidi wake.
Ameongeza  kuwa  mambo mengine ataongea yeye mwenyewe Edward Lowassa  atakapo pata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Kwa upande wake  Dk Emmanuel Makaidi  ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NLD amesema Lowassa ni mtu safi kwa kuwa tangu alipojiuzulu hajashitakiwa  hivyo wanamkaribisha kwa mikono miwili katika umoja huo wa katiba ya wananchi UKAWA muda wowote kuanzia sasa.
Katika hatua nyingine umoja huo umesema unatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais mwanzoni mwa mwezi agosti kwa mbwembwe na sherehe kubwa  ,hivyo umewataka wananchi kuisubiri kwa hamu siku hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: