Lowassa akaribishwa rasmi UKAWA


Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu jijini Dar es salaam.
Wenyeviti wa vyama vinavyounda UKAWA wakizungumza na waandishi wa Habari leo.
Wenyeviti wa vyama vinavyounda UKAWA wakizungumza na waandishi wa Habari leo.
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umesema unamualika Waziri mkuu Mstaafu Edward Lowassa kujiunga na umoja huo  ili kukiondoa chama tawala cha Mapinduzi CCM.
Akizungumza na waandishi wa Habari muda huu makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dares salaam Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia amesema  Lowassa anakaribishwa katika umoja huo kwa kuwa ana uwezo mkubwa  wa kuhamasisha umma kuikataa CCM yenye mfumo usiotenda haki.
Ameongeza kuwa Lowassa ni mchapa kazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa kiutendaji katika majukumu anayokabidhiwa.
Alipoulizwa kuwa Lowassa atakuwa mgombea Urais Mbatia amesema kila chama kina utaratibu wake  hivyo mchakato ukishakamilika  atatangazwa mgombea urais wa UKAWA mmoja  mwanzoni mwa mwezi agosti.
Kumekuwepo na taarifa kuwa Lowassa ana mpanga wa kutumkia Upinzani na hivyo basi huenda akatimkia Upinzani na kupata ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja huo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: