Watu
watatu wamelazwa katika hospitali teule ya Shirati wilayani Rorya baada
ya kujeruhiwa vibaya katika ugomvi ambao unadaiwa kuhusishwa na kampeni
za kisiasa za wagombea wa ubunge wa chama cha mapindizikatika jimbo la
Rorya mkoani Mara.
Mmoja
wa majeruhi wa tukio hilo, amesema walishambuliwa na chupa huku
wakitishiwa kukatwa mapanga muda mfupi baada ya kumalizika mkutano wa
kampeni za CCM katika eneo hilo.
Hata
hivyo mwenyekiti wa CCM wilayaya Rorya Bw Samwel Kiboye, amekiri kupata
taarifa hizo kuhusu wafuasi wa mmoja ya wagombea kununuliwa silaha za
jadi kwa ajili ya kuwashambulia vijana wa wagombea wengine na kusema
mbali na tukio hilo kufikishwa katika vyombo vya dola pia chama hicho
kitachukua hatua kali kwa wahusika huku mmoja wagombea Mh Lameck Airo
akitishia kujitoa kugombea ubunge endapo vitendo hivyo havitadhibitiwa.
0 comments:
Post a Comment