Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Ojuku Abraham
SINTOFAHAMU! Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama
vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD sasa upo njia panda kuhusu
ujio wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa anayesemwa kutaka kutimka
kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dkt. Willibrord Slaa.
Habari kutoka ndani ya vyama hivyo zinasema, tangu kukatwa kwa Lowassa
katika kuwania kwake kuteuliwa kuwa mgombea urais, kumekuwa na shinikizo
kubwa kutoka kwa watu mbalimbali, wanaotaka kada huyo wa chama tawala
anayetajwa kuwa na wafuasi wengi ajiunge na Chadema, ili awanie nafasi
hiyo kwa tiketi ya Ukawa.
Prof. Ibrahim lipumba.
“Kuna vikao vingi ndani ya vyama hivyo kiasi kwamba wameshindwa kumtaja
mgombea wao ili kusubiri kwanza wajue hatima ya Lowassa. Inadaiwa kuwa
Chadema imegawanyika, kwani baadhi ya vigogo wanamtaka kada huyo wa CCM
na wengine wanapinga, CUF wanamtaka hata sasa hivi. Ninachoweza
kukuambia ni kwamba ndani ya Ukawa, hali ni tete, haieleweki,” kilisema
chanzo chetu kilichopo ndani ya umoja huo.
Licha ya viongozi wakuu, chanzo hicho kilidai kuwa hata makada wa
kawaida wa Chadema, chama kinachodaiwa kuwa ndiyo lengo la Lowassa,
wamegawanyika, kwani wapo wanaomuona kama mwenye mtaji mkubwa kisiasa,
huku wengine wakimuona ni doa litakalowapa tabu kuliondoa.
James Mbatia.
Shinikizo la Lowassa linatokana na ukweli kuwa kwa muda mfupi tangu jina
lake liondolewe na Kamati ya Maadili ya CCM kiasi cha kutowasilishwa
katika kikao cha Kamati Kuu, makundi mbalimbali ya makada wamejiengua
kutoka chama tawala na kujiunga na Chadema, wakiwemo zaidi ya madiwani
kumi na nne na wenye viti wa vijiji wilayani Monduli.
Akizungumzia kuhusu uwezekano wa Lowassa kujiunga na Chadema,
mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema kilichopo ni uvumi tu
ambao hata wao wamekuwa wakiusikia hivyo hana cha kuzungumzia.
0 comments:
Post a Comment