FILIKUNJOMBE AHASA AMANI,UPENDO NA UTULIVU NDANI ZA UMOJA WA AKINA MAMA CCM

 

LUDEWA

Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa njombe kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) Mh.Deo Filikunjombe ambae kwa sasa anamaliza muda wake wa uongozi kwa kipindi cha muda wa miaka 5 na kuomba ridhaa kwa mara nyingine kwa wananchi amewataka wanawake wilayani hapa kuchagua viongozi bora na wachapakazi hasa madiwani wa viti maalumu ili aweze kushirikiana nao kikamilifu kwa lengo la kuleta maendeleo wilayani hapa endapo atapita kwa awamu ya pili.


Ameyasema hayo mapema hii leo katika mkutano wa umoja wa kinamama (UWT) uliofanyika katika ukumbi wa CCM Ludewa mjini uliokuwa na lengo la kuchagua madiwani wa Viti maalumu katika tarafa tano za wilaya ya Ludewa.


Aidha amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 5 ya uongozi wake amekumbana na baadhi ya changamoto ikiwemo ni pamoja na baadhi ya madiwani kutokuwa na ushirikiano na yeye kama mbunge hivyo kwasasa anawaomba wanawake hao kuchagua madiwani ambao watakuwa na lengo kubwa la kubadili maisha ya wananchi kwakuchochea kasi ya maendeleo.

Pia amesema kuwa kwasasa anamaliza muda wake akiwa kama mbunge wa jimbo la Ludewa lakini bado ana lengo na nia kubwa ya kuzidi kuiongoza wilaya ya Ludewa ili aweze kukamilisha baadhi ya miradi ya maendeleo aliyoianzisha katika kipindi cha uongozi wake.

Hata hivyo ameutaka uongozi wa UWT wilayani hapa  kuita mikutano ya wanawake mara kwa mara na kuacha tabia ya kuwaita wanawake hao kwa kipindi cha uchaguzi ili kuweza kuwa pamoja na wanachama wa CCM.

VIA  BEST FM RADIO LUDEWA
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: