Mafahari wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’.
MAFAHARI wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’
wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye
mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile hawajuani.
Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kiliusoma ‘mchezo’ mwanzo mwisho,
Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe
wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao
walifika na kukaa meza nyingine.
Aunt Ezekiel.
Habari zinazidi kudai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na
Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt
tangu ajifungue.
“Yaani kwa kweli hakuna hata mmoja aliyeamini kilichotokea pale kwa kuwa
watu wengi wanajua ni marafiki wa damu lakini kiliwashangaza watu, hata
kupeana salamu kweli? Kila mmoja aliendelea kufanya kilichompeleka,”
kilisema chanzo chetu.
Mpashaji wetu huyo alizidi kumwaga ubuyu kuwa baada ya Aunt kumaliza
kula Ice Cream na kundi lake, waliinuka na kuondoka zao na kumuacha Wema
na marafiki zake.
Baada ya gazeti hili kupata habari hiyo lilimtafuta Aunt ili aweze
kuzungumzia kitendo hicho na bifu lao ambapo alikiri kuonana na Wema
lakini alisema kuwa kila mmoja alikuwa na shuguli zake eneo hilo.
“Jamani unajua kila mtu alienda kwa ajili ya kazi zake na ndiyo kama
tulivyokutana kila mmoja alikuwa yupo na taratibu zake, sioni kama ni
bifu, sina comment,” alisema Aunt.
Jitihada za kumpata Wema ambaye ametangaza nia ya kugombea ubunge mkoani
Singida kupitia viti maalum ili aweze kuzungumzia tukio hilo ziligonga
mwamba lakini hivi karibuni alizungumza na mwanahabari wetu na kukiri
kuwa kuna tatizo kati yao lakini hakutaka kuliweka wazi
0 comments:
Post a Comment