Majimboni 2015: Job Ndugai ‘amchapa’ mgombea Mwezake, azimia


Job Ndugai,pembeni ni mgombea Dickson Chilongani mara baada ya kupigwa fimbo.
Job Ndugai,pembeni ni mgombea Dickson Chilongani mara baada ya kupigwa fimbo.
Naibu Spika Job Ndugai amempiga Mgombea mwenzie Dkt. Dickson Chilongani  kwa fimbo hadi kuzimia wakati wa kampeni wa kunadi sera za ubunge leo.

Tukio hilo limetokea leo  majira ya saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa ambapo watia nia wa Ubunge walikuwa wakinadi sera zao.
Katika tukio hilo Mgombea mmoja  mkazi wa Kongwa Bw. ngatunga alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini  na  jimbo halija  faidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini.
Mara baada ya kauli hiyo   Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonyesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi mbele ya wananchi.
Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla Ngugai  alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr. Joseph Chilongani ameshika simu akiwa anamrekodi kwa kuvunja taratibu.
Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia “Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani.”
Ndugai alimfuata na kumpiga na fimbo ndipo mgombea huyo alipozimia.
Baada ya tukio hilo Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu wengine  walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiza hospital baada ya kupata PF 3 toka polisi.
Kufuatia tukio hilo Ndugai aliondoka katika eneo hilo  ghafla  kwa kutumia gari lake la kutembelea.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: