Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ametangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Ukumbi wa Mwl. Nyerere Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.Aidha, katiba hotuba yake Mwigulu pia amempongeza Rais Kikwete kwa kumuamini na kumteua katika nyadhifa mbalimbali ambapo katika hotuba ameyataja mambo matatu katika uongozi wake endapo atachaguliwa kuwa rais ambayo ni , Kutaka Mabadiliko, kujua mbinu za mabadiliko pamoja na utayari wa kufanya mabadiliko.Ameamua kutangaza nia akiwa mkoani Dodoma ili kuondoa dhana ya ‘ukwetu kwetu’ iliyozoeleka miongoni kwa viongozi. Ameeleza jinsi anavyozijua fika shida za Watanzania na umasikini walionao amesema hajausomakwenye vitabu bali ni maisha aliyoyapitia.Wananchi,wananafunzi pamoja na wageni mbalimbali wamehudhuria kwa wingi katika mkutano huo uliomalizika majira ya saa kumi na mbili za jioni.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment