Kusimamishwa kwa PSSI linafuatia mgogoro kati ya PSSI na wizara ya Vijana na Michezo ya Indonesia kuhusu vlabu gani nchini humo zishiriki Ligi Kuu nchini humo na kupelekea ligi hiyo kusimamishwa (ISL).FIFA imezipa pande hizo mbili hadi tarehe 29 Mei kutatua mgogoro huo, tarehe ambayo imepita kabla ya ufumbuzi kupatikana na hivyo kupelekea rungu kushushwa kwa PSSI.Adhabu hiyo ya FIFA itakuwa namadhara hasa kwa Indonesia hasa ikikumbukwa kuwa ni wiki ijayo nchi hiyo ilikuwa iumane na Taiwan katika mechi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia.Hata hivyo Indonesia imeruhusiwa kushiriki michezo ya nchi za Asia ya Kusini Megharibi zinazofanyika nchini Singapore.“Kamati Tendaji imeamua kusimamisha Shirikisho la Mpira la Indonesia (PSSI) mara moja hadi PSSI litakapotimiza wajibu wake chini ya ibara 13 na 17 za kanuni za FIFA”, habariya FIFA imesema.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment