Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba 2015.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Chikawe amesema akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo ataendeleza mapambano zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini pamoja na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa maendeleo.
Aidha,Waziri Chikawe ameongozana na mke wake pamoja na wapambe mbalimbali walikuwa wakimshangilia wakati wa kujibu maswali ya Waandishi wa Habari katika wa ukumbi wa Mkutano mkuu wa NEC.
0 comments:
Post a Comment